Lugha Nyingine
Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini watoa msaada wa vifaa muhimu kwa wanawake na mabinti (2)
![]() |
| (Picha inatoka tovuti ya Ubalozi wa China katika Sudan Kusini) |
Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa msaada wa vifaa vya heshima kwa wanawake na mabinti wanaoishi katika mazingira magumu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, na kuthibitisha tena ahadi ya China ya kuunga mkono maendeleo ya wanawake nchini humo.
Msaada huo, uliotolewa kwa ushirikiano na Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) na Wizara ya Jinsia, Watoto na Ustawi wa Jamii ya Sudan Kusini, unalenga kuboresha mazingira ya maisha na hadhi ya wanawake na mabinti wenye mahitaji.
Waziri wa Jinsia, Watoto na Ustawi wa Jamii ya Sudan Kusini, Nuna Rhoda Rudolf Ndefu ameishukuru serikali ya China na UNFPA kwa msaada huo, akisema ni mchango muhimu katika kulinda wanawake na mabinti walio hatarini.
Naye Balozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Qiang, amesema wanawake na mabinti ni wachangiaji muhimu katika ustaarabu wa binadamu, na kuendeleza haki na ustawi wa wanawake ni wajibu wa pamoja wa jamii ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




