Kazi ya kumimina zege kwenye boriti la mnara mkuu wa mashariki wa daraja la barabara-reli la Fuchimen yakamilika mkoani Zhejiang, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2026
Kazi ya kumimina zege kwenye boriti la mnara mkuu wa mashariki wa daraja la barabara-reli la Fuchimen yakamilika mkoani Zhejiang, China
Picha iliyopigwa Januari 25, 2026 ikionyesha mjenzi akifanya kazi kwenye sehemu ya kumimina zege kwenye boriti la mnara mkuu wa mashariki wa daraja la reli na barabara la Fuchimen kwenye Reli ya Ningbo-Zhoushan ya mji Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Kazi ya kumimina zege kwenye boriti la mnara mkuu wa mashariki wa daraja la reli na barabara la Fuchimen kwenye njia ya Reli ya Ningbo-Zhoushan katika Mji wa Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China imekamilishwa vizuri jana Jumapili, ikimaanisha mafanikio makubwa katika ujenzi wa muundo mkuu wa mnara mkuu huo na kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi unaofuatia wa mfumo mzima wa staha ya daraja.

Daraja hilo la reli na barabara la Fuchimen linaunganisha Visiwa vya Zhoushan na Fuchi na ni moja ya miradi muhimu ya Reli ya Ningbo-Zhoushan. Daraja hilo lina urefu wa mita takriban 1,726 na umbali kati ya nguzo kuu mbili wa mita 388, likiwa na reli yenye njia mbili na barabara kuu ya njia sita za magari vinavyopangwa kwenye ngazi sawa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha