Lugha Nyingine
Wajasiriamali wanawake waonyesha vyakula vitamu na kukuza utalii kupitia biashara ya mtandaoni katika Mji wa Jiande, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2026
Mwishoni mwa wiki siku ya Jumamosi, shughuli yenye kaulimbiu ya kutangaza utamaduni na utalii wa Mji wa Jiande ilizinduliwa mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. Wajasiriamali wanawake kutoka maeneo 16 ya mji huo wa Jiande walileta kwa umma aina mbalimbali za vyakula vitamu na bidhaa za kilimo za kienyeji zilizotengenezwa kwa mikono kama vile baozi za tofu, mayai, stroberi, mbegu za lotus, chai, na samaki waliokaushwa.
Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo wa Jiande umesaidia wanawake wenyeji kupata ajira nyumbani kupitia biashara ya mtandaoni na matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, hali ambayo imeongeza sana mapato ya wanawake.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




