Lugha Nyingine
Kutoka Jangwani hadi Baharini: Nishati ya upepo yaunda msingi wa mageuzi ya kijani ya China (3)
![]() |
| Picha iliyopigwa Agosti 8, 2024 ikionyesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa upepo kwenye Eneo la Mafuta la Lamadian mjini Daqing, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Zhang Tao) |
BEIJING - China ni nchi yenye nishati nyingi za upepo duniani. Kutoka Jangwa la Gobi hadi baharini, nishati ya upepo inaunda msingi wa mpito wa nchi hiyo kuelekea muundo wa maendeleo ulio safi na endelevu zaidi.
Kwa miaka 15 mfululizo, China imekuwa ya kwanza duniani katika uwezo wa kuzalisha umeme kwa upepo kwa mitambo iliyofungwa. Hadi kufikia mwisho wa Novemba 2025, jumla ya uwezo wake huo ulikuwa umezidi kilowati milioni 600, ukizidi kwa mbali ule wa taifa lingine lolote, takwimu rasmi zinaonesha.
Kwa kuwa na mashamba makubwa ya nishati ya upepo ya bara katika maeneo yake ya kaskazini na magharibi na miradi inayopanuka kwa kasi ya nishati ya upepo baharini katika pwani ya mashariki, nishati ya upepo ya China si tu kwamba hutoa umeme safi kwa mamilioni ya kaya lakini pia inabeba jukumu muhimu katika kupunguza utoaji wa kaboni.
Nje ya mipaka yake, China imechangia kikamilifu mafanikio yake ya kijani. Wakati wa kipindi cha 2021-2025, nishati ya upepo na bidhaa za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua ambazo China iliuza nje zimesaidia kupunguza tani takriban bilioni 4.1 za utoaji wa kaboni katika nchi zingine, takwimu hizo rasmi zinaonyesha.
Ikichochewa na mfumo mkubwa zaidi wa nishati mbadala duniani, uvumbuzi unaoendelea wa kiteknolojia na uungaji mkono mkubwa wa sera, China iko tayari kuendelea na ushirikiano wa kimataifa katika kusukuma mbele mpito duniani kuelekea mustakabali wa kijani, wenye kutoa kaboni chache, ikichangia maono ya pamoja ya dunia safi na yenye kupendeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




