Lugha Nyingine
Wafanyakazi kwenye sehemu ya uhifadhi wa mfumo wa ishara, zana na majengo ya reli ya juu zaidi duniani ya China (5)
Sehemu ya reli ya uhifadhi wa mfumo wa ishara, zana na majengo ya Za'gya Zangbo katika Wilaya ya Amdo ya eneo la Nagqu, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China ambayo iko kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 4,886, ni sehemu ya uhifadhi wa mfumo wa ishara, zana na majengo ya reli ya juu zaidi duniani. Sehemu hiyo hukumbwa na upepo wenye nguvu kubwa na baridi kali, ambapo halijoto mara nyingi hushuka hadi nyuzi joto 30 hasi.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018, sehemu hiyo inafanya kazi za kuhifadhi na kufanya ukarabati wa zana za kutoa ishara na majengo kwenye stesheni tatu zilizoko kwenye mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari -- Tanggula Kusini, Za'gya Zangbo na Xuechama. Wafanyakazi kumi vijana kutoka makabila mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Wahan, Watibeti na Wamongolia, wanafanya kazi kwenye sehemu hiyo yenye hali gumu.
Wastani wa umri wa wafanyakazi hao ni chini ya miaka 32, ambao wanashikilia kazi zao wakikabiliana na hali mbaya ya hewa ili kuhakikisha usalama wa uendeshaji wa treni kwenye njia hiyo ya reli, na kutoa uhakikisho kwa usafirishaji wa bidhaa usio na matatizo wakati wa pilika za usafiri wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, pamoja na kuhakikisha usafirishaji usio na matatizo kwa muda mrefu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




