Lugha Nyingine
Habari picha: Miaka 20 ya kufanya kazi kwa bidii kwenye Reli ya Qinghai-Xizang ya China
Tangu Reli ya Qinghai-Xizang ilipoanza kufanya kazi kikamilifu mwaka 2006, timu ya ulinzi wa reli hiyo imekuwa ikiweka kambi katika Mji wa Nagqu wa Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, mji ulio kwenye mwinuko wa juu zaidi nchini China. Wanasimamia sehemu ya reli ya urefu wa kilomita 25, wakiwa na majukumu ya kutambua hatari zinazoweza kutokea, kuzuia watu na mifugo kuingia kwenye reli, na kushiriki katika operesheni za uokoaji baada ya ajali kutokea kwenye njia hiyo.
Kwa miaka 20, wameshinda changamoto za kwenye mwinuko wa juu na hali mbaya ya hewa. Wakati wa msimu wa ufugaji wenye pilika nyingi, wafanyakazi hao pia husaidia wafugaji wenyeji kukata sufi za kondoo na kukarabati nzio.
Katika miaka mingi iliyopita, hali yao ya maisha imeboreka kwa kiwango kikubwa. Majengo yenye maji ya bomba, umeme na vifaa vya kupasha joto yamekuwa mbadala wa mahema. Maeneo ya kujihifadhi pia yamejengwa kando ya njia ya doria.
Simulizi ya timu hii ni mfano mmoja tu. Kwenye Reli hiyo ya Qinghai-Xizang, wafanyakazi wengi wa ulinzi wa reli wamekuwa wakilinda usalama wa abiria kupitia kufanya kazi yao ngumu kwa bidii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




