Dereva wa treni ya mwendo-kasi ya Fuxing kutoka Xizang afuata ndoto zake kwenye Reli ya Qinghai-Xizang, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2026
Dereva wa treni ya mwendo-kasi ya Fuxing kutoka Xizang afuata ndoto zake kwenye Reli ya Qinghai-Xizang, China
Tsering akiendesha treni ya mwendo-kasi ya Fuxing kuelekea Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 27, 2026. (Xinhua/Jigme Dorje)

LHASA – Tsering, Mzaliwa wa Xigaze katika Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, mwenye umri wa miaka 31 ni dereva mdogo zaidi wa Kabila la Watibet wa treni ya Fuxing kwenye Reli ya Qinghai-Xizang.

Wakati Tsering alipokuwa na umri wa miaka 10, alijifunza kuhusu treni kutoka kwa kaka yake mkubwa ambaye alikuwa akifanya kazi katika sekta ya reli. Treni hizo zinazoelezwa kuwa za kasi na tulivu zimemvutia sana tangu wakati huo.

Katika mwaka wake wa tatu chuoni, Tsering alijiandikisha mara moja wakati kampuni ya Reli ya Qinghai-Xizang ilipokuja chuoni kwake kuajiri madereva wa treni. Akiwa mfanyakazi mpya wa kampuni hiyo, alipanda treni kutoka Lhasa hadi Xining mwaka 2017, ambayo ilikuwa safari ya kwanza ya treni maishani mwake.

Kuwa dereva wa treni ya mwendo-kasi kunahitaji kukumbuka yaliyomo kwenye vitabu kadhaa vya lugha ya Kichina sanifu (mandarin), ikiwemo maneno ya kiufundi na data za madaraja na mahandaki kwenye njia nzima ya reli.

Kwa sababu alikosa ufahamu wa kutosha wa lugha ya Kichina sanifu, Tsering mara nyingi alikuwa akijisomea hadi saa 8 au 9 usiku, na kufanya mazoezi ya kuandika baada ya kumaliza kusoma nyaraka. Hatimaye, alifaulu mitihani yote minne ya kufuzu kwa kupata leseni za madaraja ya J5, J9, J8 na J6 za udereva wa reli katika jaribio lake la kwanza, na kumfanya kuwa mwanagenzi pekee Mtibet miongoni mwa wenzake kufikia mafanikio hayo.

Katika siku ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kufunguliwa kwa Reli ya Lhasa-Xigaze, Tsering aliendesha treni ya mwendo-kasi ya Fuxing hadi mji huo alikozaliwa wa Xigaze Agosti 16, 2024, akiamini kwamba mahali kwake hapo alikozaliwa panazidi kuwa bora zaidi na zaidi.

Sasa Tsering anaishi Lhasa. Baada ya kutimiza ndoto yake ya utotoni, lengo lake linalofuata ni kupata leseni ya daraja la J7 ya udereva wa reli ya mwendo-kasi. Ndoto za Tsering zinabadilika sambamba na nyakati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha