Michezo ya Maonyesho ya Besiboli na Tamasha la Michezo la Vijana wa China na Marekani 2026 vyaanza (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2026
Michezo ya Maonyesho ya Besiboli na Tamasha la Michezo la Vijana wa China na Marekani 2026 vyaanza
Watumbuizaji wakifanya onyesho kwenye hafla ya ufunguzi wa Uhusiano na Kuliang: Michezo ya Maonyesho ya Besiboli na Tamasha la Michezo la Vijana wa China na Marekani 2026, Fuzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Juni 29, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

Michezo ya Maonyesho ya Besiboli na Tamasha la Michezo la Vijana wa China na Marekani 2026, vyenye kaulimbiu isemayo "Kurusha Mpira Kuvuka Bahari, Kukumbatia Mustakabali," vimeanza mjini Fuzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China jana Jumatatu.

Washiriki wapatao 400, wakiwemo wajumbe wa timu nane za besiboli za vijana kutoka China na Marekani, wajumbe wa "Marafiki wa Kuliang," kundi la wazao wa familia za Wamarekani ambao waliwahi kuishi Fuzhou, wanafunzi wa Shule ya Urafiki ya Flying Tigers na wawakilishi kutoka miji dada, walihudhuria shughuli hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha