Lugha Nyingine
Timu ya China yaishinda timu ya Japan na kutwaa taji la 10 la mpira wa wavu kwa wanawake katika Michezo ya Asia
Bingwa mtetezi timu ya China, jana jumanne ilipata medali yake ya 10 ya dhahabu kwenye mchezo wa fainali ya mpira wa wavu kwa wanawake kwenye Michezo ya Asia, kwa ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Japan.
Timu hizo mbili zilibadilishana nafasi ya kuongoza mapema katika seti ya kwanza. Katikati ya seti, na China ilisonga mbele polepole na kupata ushindi wa pointi 25-19. Timu ya China ilidumisha uongozi mdogo katika seti ya pili. Pande zote mbili ziliongeza nguvu, zikiandaa mikusanyiko kadhaa mirefu kabla ya China kufunga seti 25-20.
Mshambuliaji wa timu ya China Bi. Wu Mengjie alisema, "Kwa kweli tulikuwa tumejiandaa kwa magumu na tulitarajia kwa kuwa tulijua kuwa hali kama hiyo inaweza kutokea. Kwa hivyo tulipokutana na ugumu, tulibaki kuwa watulivu na makini."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




