Kazi ya kufunga nyaya za kuvuka Mto Changjiang ya mradi wa kusafirisha umeme yakamilishwa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2026
Kazi ya kufunga nyaya za kuvuka Mto Changjiang ya mradi wa kusafirisha umeme yakamilishwa
Picha ikionesha mafundi umeme wakifanya kazi kwenye eneo la mradi wa kusafirisha umeme wa mkondo wa moja kwa moja wenye volteji ya juu sana (UHVDC) ya ±800kV pembeni ya Mto Changjiang huko Wuhu mkoani Anhui, mashariki mwa China, Oktoba 26, 2026. (Picha na Zheng Xianlie/Xinhua)

Kazi ya kufunga nyaya za kuvuka Mto Changjiang ulio mpana katika mradi wa kusafirisha umeme wa mkondo wa moja kwa moja wenye volteji ya juu sana (UHVDC) ya ±800kV imekamilishwa jana Jumatatu huko Wuhu, mkoani Anhui, mashariki mwa China.

Mradi huo una urefu wa jumla wa kilomita 2,370 kutoka Mkoa wa Gansu kaskazini-magharibi mwa China hadi Mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China. Mara utakapokamilika na kuanza kufanya kazi, utaweza kusafirisha umeme kwa bilioni zaidi ya 36 za kilowati-saa (kWh) kwenda Mkoa wa Zhejiang kwa mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha