(Picha inatoka CRI.) Rais Xi Jinping wa China leo ametoa hotuba kwa njia ya video katika ufunguzi wa mkutano wa 139 wa wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa.
Picha iliyopigwa Januari 10, 2022 ikionesha vifaa vya kudhibiti janga la UVIKO-19 katika Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022 huko Beijing. (Xinhua/Xu Zijian) BEIJING - Huang Chun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kuzuia na Kudhibiti Janga la Virusi vya Korona ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 amesema kwamba, haina haja ya kudanganya matokeo ya vipimo vya UVIKO-19, na China kamwe haitafanya hivyo.
Mwenge wa Olimpiki kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 ukioneshwa kwenye Mnara wa Olimpiki huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Oktoba 20, 2021. (Xinhua/Wang Yong) BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Hua Chunying ametangaza Ijumaa ya wiki hii kwamba, kuanzia Februari 4 hadi 6, Rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, na kufanya hafla ya kuwakaribisha wakuu wa nchi mbalimbali duniani, wakuu wa serikali, wajumbe wa familia za kifalme na wakuu wa mashirika ya kimataifa watakaohudhuria sherehe hiyo, na kufanya shughuli mbalimbali husika za uhusiano wa pande mbili.
BEIJING - Vijiji vya Olimpiki kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 cha eneo la Yanqing, mjini Beijing na Zhangjiakou, Mkoa wa Hebei vilifungua milango yao kwa wanamichezo na maafisa wa timu kwa ajili ya Michezo hiyo siku ya Alhamisi ya wiki hii. Zhang Guannan, mfanyakazi wa timu ya uendeshaji wa Kijiji cha Olimpiki cha Beijing, amesema kijiji hicho kitawapokea wanamichezo 1,000 na maafisa wa timu kutoka nchi na kanda 44.