BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amemwambia Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) Thomas Bach ambaye yuko ziarani nchini China kuwa China iko tayari kuwasilisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi iliyo rahisi, salama na murua. Xi amekutana na Bach, kwenye Jumba la Wageni la Taifa la Diaoyutai mjini Beijing, siku 10 kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Michezo hiyo mnamo Februari 4.
Mazoezi ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 yamefanyika kwenye Uwanja wa Taifa uitwao "Kiota cha Ndege," Januari 22, 2022. Takriban washiriki 4,000 walihusika katika mazoezi ya kila tukio la sherehe ya ufunguzi, wakijiandaa kwa sherehe ya ufunguzi itakayofanyika Februari 4.
Kijiji cha Michezo ya Olimpiki cha Zhangjiakou ( Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika hapa Beijing na huko Zhangjiakou, ndiyo maana kuna vijiji viwili vya michezo hiyo ) kilifunguliwa Januari 23 na kukaribisha kundi la kwanza la wakazi. Zaidi ya watu 40 wa ujumbe wa watangulizi wa michezo hiyo kutoka Australia, Uingereza, Kanada na nchi na kanda nyingine walifika na kukaa huko.
(Picha inatoka ukurasa wa akaunti ya Facebook ya Rais Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.