Kwa kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imekaribia, majaribio ya mwisho ya zana na vifaa na mazoezi ya mwisho ya mchakato mzima wa michezo hiyo yanafanyika kwenye uwanja wa utoaji wa medali wa Beijing, uwanja huo uko karibu na Uwanja wa Michezo wa Taifa “Kiota cha Ndege”.
BEIJING -- Afisa Mwandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Kunming Jumatano ya wiki hii ameelezea matumaini yake kwamba marafiki kutoka vyombo vya habari vya kimataifa watashiriki kutoa habari chanya za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing na kuonesha Michezo hiyo ya Olimpiki ya "kuvutia, ajabu na bora". Huang Kunming, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China (CMG).
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alisema Januari 26 kuwa upande wa China unasifu sana uungaji mkono wa Rais Vladimir Putin wa Russia kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Ameeleza matumaini yake kuwa wanamichezo wa nchi mbalimbali wakiwemo pamoja na wanamichezo wa Russia watapata mafanikio bora na kung'ara kwenye uwanja wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema anaamini kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itapata mafanikio makubwa na kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kati ya vijana wa nchi mbalimbali zikiwemo Korea Kusini na China.