(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.) Akijibu swali kuhusu wasiwasi uliooneshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchi za nje kuhusu kama uhuru wa vyombo vya habari kuandika habari wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing utaathiriwa na hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Januari 13 alisema, China kama kawaida italinda haki halali za waandishi wa habari na mashirika ya habari ya kigeni nchini China kwa mujibu wa sheria, na kuwezesha waandishi wa habari kuandika kwa urahisi habari za Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Bejing kwa mujibu wa mkataba wa mji mwenyeji wa michezo hiyo.
BEIJING – Kufuatia kufungua duka jipya katika Kituo cha Michezo ya Barafu mjini Beijing, chapa ya vifaa vya mpira wa magongo kwenye barafu ya Marekani TRUE imekaribishwa sana na vijana wanaojifunza mchezo huo. Duka hilo lililofunguliwa Oktoba 2021, linatoa huduma za manunuzi ya vifaa "vyote kwa pamoja" kwa vijana wanaojifunza mchezo huo katika kituo hicho ili wasilazimike kwenda maeneo mengine mjini Beijing kutafuta moja ya vifaa vya mchezo huo kama vile helmeti, glavu, sketi na vijiti.
BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema kwamba, nchi hiyo itaonesha kwa Dunia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ambayo ni ya kipekee na ya kuvutia, na kuwafanya washiriki wote kuhisi furaha na kuleta mshikamano, imani na nguvu zaidi duniani. Wang Wenbin ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi ya wiki hii ambapo amebainisha kuwa katika siku ya kwanza ya kazi baada ya mapumziko ya Mwaka Mpya, Rais Xi Jinping wa China kwa mara nyingine tena alikagua maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022, tukio ambalo linadhihirisha kikamilifu umuhimu mkubwa unaopewa na China katika maandalizi hayo.
Siku hiyo, shughuli ya kuonesha Mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 ilifanyika katika Mji wa Harbin, Mkoa wa Hei Longjiang. Baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo, Mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi utaoneshwa katika Miji ya Daqing na Qiqihar kwa mfululizo.