Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping Desemba 4, akitembelea Uwanja wa Taifa wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji, Kituo Kikuu cha vyombo vya habari cha Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing, Kijiji cha Wanamichezo cha Beijing, Kituo cha Usimamizi na Uratibu wa michezo hiyo na Kituo cha mazoezi cha mradi wa theluji na barafu, ambapo alifahamishwa hali halisi ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, kuwatembelea wanamichezo, makocha, wasimamizi, wahudumu, watafiti wa kisayansi, waandishi wa habari na watu wanaojitolea, na kuwapa salamu za mwaka mpya.
Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 ukioneshwa kwa umma katika Bustani ya Shougang huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 13, 2021. (Xinhua/Zhang Chenlin) BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amethibitisha kuwa China imepokea maombi ya viza kutoka kwa wafanyakazi husika wa Marekani ya kuhudhuria Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.
Kuanzia Tarehe 28 hadi Tarehe 31, Desemba, Kituo cha Kitaifa cha Michezo Miwili ya Majira ya Baridi kilichoko Eneo la Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi la Zhangjiakou, kitaanza wiki ya mazoezi ya wanamichezo wa nchi mbalimbali, ambayo ni shughuli ya mwisho katika mfululizo wa shughuli za majaribio za“Tukutane Beijing” za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Hivi sasa maandalizi mbalimbali ya uwanja huo yamekamilika.
BEIJING - Naibu Waziri Mkuu wa China Han Zheng amesisitiza haja ya kuweka kipaumbele katika kuzuia na kudhibiti janga la UVIKO-19 ili kufanikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Mwaka 2022 "rahisi, salama na ya kifahari". Han, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa kikosi kazi kinachosimamia maandalizi ya Michezo ya Omlimpiki ya Mjira ya Baridi ya Beijing 2022, amesema hayo Jumanne ya wiki hii wakati wa ziara ya ukaguzi wa viwanja kadhaa huko Beijing, ukiwemo Jumba la Taifa la Mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye barafu.