Nembo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 (Kushoto) na Nembo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing 2022. (Kamati ya maandalizi ya Beijing 2022/Kutolewa kupitia Xinhua) BEIJING - Ikiwa imesalia chini ya miezi miwili kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kuanza, Kamati ya Maandalizi, pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) zimechapisha toleo la pili la mwongozo juu ya hatua za kukabiliana na UVIKO-19 wakati wa michezo hiyo.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, alfajiri ya Jumatatu (leo), mashine nne za kutengeneza theluji, taa za usiku za jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji zimewashwa, hali ambayo inaonesha utoaji wa umeme kwenye uwanja huo wa michezo umefikia kigezo cha matumizi wakati wa mashindano, na jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang limeanza rasmi kutengeneza theluji. Jukwaa la kuteleza na kuruka juu ya theluji la Bustani ya Shougang liko ndani Bustani mpya ya Shougang katika Eneo la Shijinshan la Beijing.
Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres amesema Alhamisi ya Wiki hii kwamba Katibu Mkuu Guterres amepokea na kukubali mwaliko wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki (IOC) wa kushiriki kwenye sherehe za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022.
BERLIN - Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach amesema kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 haipaswi kutumiwa kwa kuongeza hali ya mivutano duniani na kwamba ushiriki wa wanamichezo ni makubaliano ya kimataifa. Bach ameelezea wasiwasi wake kuhusu ushiriki wa wanamichezo baada ya Marekani kutangaza kutotuma maafisa wa serikali kuhudhuria mashindano hayo yatakayofanyika Beijing mapema Mwaka 2022 kwa kisingizio cha haki za binadamu.