NEW YORK – Konsela mkuu wa ubalozi wa China katika Mji wa New York nchini Marekani Huang Ping amesema kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 siyo tu itaongeza maelewano na urafiki kati ya nchi na sehemu mbalimbali, lakini pia itaongeza imani na matumaini kwa binadamu kushirikiana katika kukabiliana na changamoto. Katika Makala yake iliyochapishwa wiki hii na Gazeti la Philadelphia Inquirer, Huang amewaalika wanamichezo kutoka Marekani na duniani kote kukusanyika pamoja mjini Beijing, kutimiza ndoto yao ya Olimpiki, kufahamu utamaduni wa China, na kusalia kumbukumbu zisizosahaulika za Olimpiki ya Majira ya Baridi maishani yao.
BEIJING – Toleo la kwanza la Kitabu kinachoelezea hatua za kupambana na UVIKO-19 kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing mwaka 2022 kimetolewa leo Jumatatu. Kitabu hicho cha mwongozo, kilichochapishwa kwa pamoja na waandaaji wa Beijing 2022, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) kinatoa matoleo tofauti kwa wanariadha na maafisa wa timu pamoja na wahusika wengine ikiwa ni pamoja na familia ya wanariadha, vyombo vya habari, Mashirikisho ya Kimataifa (IFs) na maafisa wa kiufundi.
Shughuli ya wakati wa siku 100 zinazobaki kabla ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing ya mwaka 2022 ilifanyika kwa shangwe Beijing tarehe 26, Oktoba. Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama, ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China na kiongozi wa kikundi cha uongozi wa kazi ya Michezo ya Olimpiki ya 24 ya majira ya baridi Bw.
Leo asubuhi, moto wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing mwaka 2022 umefika hapa Beijing, na hafla ya kuukaribisha imefanyika kwa shangwe. Halafu, mpango wa kuonesha moto huo na wa kupokezana kwa mwenge ulitangazwa.