人民网首页

Habari

Msemaji wa China: Marekani "italipa gharama" kwa hatua zake zisizo sahihi dhidhi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian ameeleza kuwa Marekani "italipa gharama” kwa ajili ya hatua zake zisizo sahihi". Msemaji huyo amesema hayo Jumanne ya wiki hii wakati alipozungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na China kwa kujibu taarfia iliyotolewa na Ikulu ya Marekani kwamba nchi hiyo haitatuma ujumbe wowote wa kidiplomasia au rasmi kuhudhuria Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022.

Picha iliyopigwa Novemba 30, 2021, ikionesha mandhari mbalimbali za Bustani ya Shougang katika Wilaya ya Shijingshan, Beijing. (People's Daily Online/Peng Yukai)

Ndani ya Bustani ya Shougang: Utulivu kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

Bustani ya Shougang, ni eneo la kinu cha chuma lililogeuzwa kuwa Maeneo yenye shughuli za Kitamaduni na Michezo katika Wilaya ya Shijingshan Magharibi mwa Beijing. Kwa sasa imekuwa Makao Makuu ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kwa Walemavu ya Beijing Mwaka 2022.

Putin akubali kwa furaha mwaliko wa kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Kwa mujibu wa ripoti, Msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov hivi karibuni alisema kuwa Rais Vladimir Putin amepokea mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China wa kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 , na baada ya Russia na China kukubaliana katika masuala yote, pande hizo mbili zitatangaza kwa pamoja habari husika. Siku ya Jumatatu ya wiki hii, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alipojibu maswali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa kushiriki matukio makubwa kwa pamoja ni desturi nzuri ya miaka mingi kati ya China na Russia.

China iko tayari kuionesha Dunia Michezo ya Olimpiki inayoandaliwa kirahisi, yenye usalama na ya murua

Hivi karibuni, serikali mbalimbali na kamati za michezo ya Olimpiki za nchi mbalimbali duniani zimeeleza matarajio na uungaji mkono kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022. Aidha, ofisi za ubalozi za nchi kadhaa zimefanya shughuli mbalimbali zinazohusu michezo hiyo.

Iliyopita18 19 20 21 22 Inayofuata