人民网首页

Habari

Timu ya China yapata medali mbili za dhahabu tena kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi

Machi 9, Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ilifikia siku yake ya tano ya mashindano. Kwenye mashindano ya mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kutumia magongo (kwa kukaa) ya michezo hiyo ya Olimpiki, Zheng Peng na Yang Hongqiong walishinda medali za dhahabu kwa Mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanaume na kwa wanawake.

(Picha ilipigwa na Weng Qiyu/People's Daily Online)

Timu ya China yashinda nafasi tatu za mbele za mchezo wa kuteleza kwenye theluji kwa ubao kwa wanaume katika Michezo ya Paralimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Tarehe 7, Machi, fainali ya mchezo wa mbio za kuteleza kwenye theluji kwa ubao na kupita vizuizi wa kiwango cha UL ilifanyika. Mwishowe mwanamchezo wa Timu ya China Ji Lijia alinyakua ubingwa, Wang Pengyao alipata nafasi ya pili, na Zhu Yonggang alipata nafasi ya tatu.

Rais wa China ajibu barua ya rais wa IOC Thomas Bach

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua iliyoandikwa na rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach. Katika barua yake, Rais Xi ameeleza kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 imemalizika kwa mafanikio, na China imetekeleza kikamilifu ahadi yake kwa kuandaa Michezo ya Olimpiki iliyozingatia kubana matumizi ya fedha, usalama na mizuri, na kusifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.

(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 zafanyika Beijing

Sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 zimefanyika leo usiku katika Uwanja wa Michezo wa Taifa wa China. Rais Xi Jinping wa China na Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Walemavu ya Kimataifa Parsons wamehudhuria ufunguzi huo.

Iliyopita1 2 3 4 5 6 Inayofuata