人民网首页

Habari

China yashika kasi Kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 huku ikiongeza medali za dhahabu

Mwanamichezo wa timu ya China Qi Guangpi. (Picha/Xinhua) BEIJING - China ilipanda hadi nafasi ya nne kwenye jedwali la orodha ya medali za Olimpiki ambazo nchi washiriki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 zimeshinda baada ya mwanamichezo mkongwe wa kuteleza kwenye theluji na kuruka hewani kwa ubao Qi Guangpu kuipatia nchi mwenyeji wa michezo hiyo medani yake ya saba ya dhahabu Jumatano wiki hii.

Chapa ya Uswisi ya Stockli yaona Michezo ya Olimpiki ya Beijing kama kichocheo cha biashara yake nchini China

GENEVA – Kampuni ya vifaa vya Michezo ya Uswisi Stockli ambayo ni mtengenezaji mkuu wa vifaa vya michezo ya kuteleza kwenye theluji imesema Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imeongeza nguvu mpya katika biashara yake nchini China na kwamba inatarajia kuona ukuaji wa biashara yake kwa tarakimu mbili katika miaka michache ijayo. "Tunaamini kwamba hata baada ya Olimpiki, mwelekeo wa ukuaji wa michezo ya majira ya baridi nchini China utaendelea," Christian Gut, Afisa Mkuu wa mauzo na masoko katika Kampuni hiyo ya Stockli ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.

(Picha inatoka People's Daily Online.)

Wafanyakazi walinda kwa makini kwa pande zote usafirishaji salama wa treni za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Reli ya Mwendokasi ya Beijing-Zhangjiakou inabeba jukumu la usafirishaji wa kuunganisha maeneo matatu ya mashindano ya michezo ya Beijing na Zhangjiakou, ili kuhakikisha huduma ya usafirishaji wakati wa siku za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Kila usiku wa manane , wafanyakazi wa treni za reli hiyo wanafanya upimaji kwa pande zote juu ya treni hizo, na kufanya jitihada zote kulinda usafiri salama wa treni kwa ajili ya mashindano ya michezo ya Olimpiki.

Mchezaji wa Timu ya China Su Yiming (Picha/Xinhua)

Su Yiming apata medali ya dhahabu kwenye mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kutumia ubao na kuruka hewani kwenye jukwa kubwa kwa wanaume

Februari 15, kwenye fainali ya mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kutumia ubao na kuruka hewani kwenye jukwaa kubwa kwa wanaume katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, mchezaji wa Timu ya China Su Yiming alitwaa medali ya dhahabu. Hii ni ya medali yake ya pili baada ya kupata medali ya fedha kwenye mchezo wa kuteleza kwenye theluji katika Mteremko kwa ubao kwa Wanaume kwenye michezo hiyo ya Olimpiki.

Iliyopita4 5 6 7 8 9 Inayofuata