人民网首页

Habari

Zhangjiakou mkoani Hebei yafanya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imemalizika siku chache zilizopita, na viwanja vya vya michezo vya Yunding katika eneo la mashindano la Zhangjiakou mkoani Hebei vimeingia haraka kwenye kipindi cha maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi, ambayo itafanyika hivi karibuni. (Mpiga picha:Wu Diansen/Tovuti ya Picha ya Umma).

Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing yaundwa

Wachezaji wakihudhuria mkutano wa uhamasishaji wa Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing katika Kituo cha Usimamizi wa Michezo ya Walemavu cha China cha eneo la Shunyi, Beijing Februari 21. (Cai Yang/Xinhua) Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing imeundwa hapa Beijing Februari 21.

China yapata mafanikio ya kusisimua Kwenye Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing 2022

Gao Tingyu, mbeba bendera wa Ujumbe wa Olimpiki wa Timu ya Jamhuri ya Watu wa China, akitembea kuongoza wenzake wakati wa sherehe za kufunga Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa, Februari 20, 2022. (Xinhua/Ju Huanzong) BEIJING - China imejinyakulia medali tisa za dhahabu na medali 15 kwa jumla katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, idadi ambayo imeweka rekodi ya juu kwa Timu ya China kushinda medali nyingi zaidi katika Olimpiki moja ya Majira ya Baridi.

Watu maarufu duniani, wanamichezo wasema Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeonesha moyo wa michezo na mshikamano

BEIJING - Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imewavutia sana maafisa, wasomi na wanamichezo kutoka kote duniani, ambao wamesema moyo wa michezo na mshikamano uliooneshwa wakati wa michezo hiyo umetoa matumaini mengi kwa jumuiya ya kimataifa. Mchezaji nyota wa Bosnia na Herzegovina Mirza Nikolajev alipata umaarufu miongoni mwa Wachina wengi baada ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, kufutia video na picha zake zinazomwonesha akikonyeza macho yake mbele ya kamera wakati wa gwaride la wanamichezo kusambaa.

Iliyopita2 3 4 5 6 7 Inayofuata