人民网首页

Habari

Mbio za mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kuanza Jumatano

BEIJING – Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 Jumanne wiki hii imetoa taarifa kwamba, mbio za Mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 zimepangwa kuanza leo Jumatano Machi 2 hadi 4, na wakimbiza mwenge 565 watashiriki katika maeneo ya mashindano ya Beijing, Yanqing na Zhangjiakou. Mkimbiza mwenge Aileen Neilson, anayetumia kiti cha magurudumu, akitazama mwenge wakati wa Sherehe za Kuwasha Moto wa asili wa Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 huko Stoke Mandeville, Uingereza, Februari 28, 2022.

 Kivutio cha Kileta bahati “Shuey Rhon Rhon” cha Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi kwenye uwanja wa kutunuku medali wa Zhangjiakou. Picha ilipigwa Februari 28.

Habari yako,Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi!

Kadiri siku ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi inavyokaribia, ndivyo mji wa Beijing unavyokamilisha maandalizi yake ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi baada ya kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Kileta bahati “Bing Dwen Dwen kimepambwa popote badala ya Kileta bahati “Shuey Rhon Rhon” kikisubiri kuwakaribisha wanamichezo wa nchi mbalimbali watakaoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi.

Moto wa asili wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing wakusanywa Mandeville, Uingereza

Moto wa asili wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing umekusanywa Februari 28 huko Mandeville nchini Uingereza. Moto huo wa asili kutoka kwenye chimbuko la Michezo ya Olimpiki ya Walemavu utaunganishwa na mioto minane mingine inayotoka maeneo matatu ya mashindano yaani Beijing, Yanqing na Zhanjiakou na kuwa moto rasmi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing.

Utaratibu wa uratibu wa ngazi ya juu katika Michezo ya Paralimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing wazinduliwa

Picha iliyopigwa Februari 10, 2022 ikionesha kileta bahati cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya walemavu ya Beijing 2022 Shuey Rhon Rhon aliyetengenezwa kwa karatasi huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing) BEIJING - Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) na Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 (BOCOG) zimefanya mkutano wao wa kwanza wa ngazi ya juu kwa njia ya video Jana Jumapili, ambapo walijadili maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya walemavu.

Iliyopita1 2 3 4 5 6 Inayofuata