人民网首页

Maoni ya Kimataifa

Rais wa IPC atangaza kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing

Andrew Parsons, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC), akihutubia ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 13, 2022. (Xinhua/Wu Zhuang) BEIJING - Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki (IPC) Andrew Parsons Jana Jumapili jioni ametangaza kufungwa rasmi kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022.

Rais wa China ajibu barua ya rais wa IOC Thomas Bach

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua iliyoandikwa na rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach. Katika barua yake, Rais Xi ameeleza kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 imemalizika kwa mafanikio, na China imetekeleza kikamilifu ahadi yake kwa kuandaa Michezo ya Olimpiki iliyozingatia kubana matumizi ya fedha, usalama na mizuri, na kusifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.

Watu maarufu duniani, wanamichezo wasema Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeonesha moyo wa michezo na mshikamano

BEIJING - Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imewavutia sana maafisa, wasomi na wanamichezo kutoka kote duniani, ambao wamesema moyo wa michezo na mshikamano uliooneshwa wakati wa michezo hiyo umetoa matumaini mengi kwa jumuiya ya kimataifa. Mchezaji nyota wa Bosnia na Herzegovina Mirza Nikolajev alipata umaarufu miongoni mwa Wachina wengi baada ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, kufutia video na picha zake zinazomwonesha akikonyeza macho yake mbele ya kamera wakati wa gwaride la wanamichezo kusambaa.

Mwanamichezo kutoka Madagascar Mialitiana CLERC afurahia kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi Beijing

Mwanamichezo kutoka Madagascar Mialitiana CLERC ni mmoja wa wanamichezo sita kutoka nchi tano za Afrika walioshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na pia ni mwanamichezo wa kwanza mwanamke kuiwakilisha Madagascar kushiriki kwenye michezo hiyo. Hii ni mara yake ya pili kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na nafasi yake kwenye mashindano ya Women's Giant Slalom imepanda kutoka 48 mwaka 2008 hadi 41 hapa Beijing.

1 2 3 4 5 6 Inayofuata