人民网首页

Maoni ya Kimataifa

Msomi wa Kenya: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imeifanya China ipate heshima duniani

(Picha inatoka CRI.) Shirika la Huduma za Utangazaji la Olimpiki (OBS) limetangaza hivi karibuni kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni michezo ya majira ya baridi inayotazamwa kwa wingi zaidi katika historia, na imewavutia watu zaidi ya bilioni mbili kwenye mitandao ya kijamii duniani.

Chapa ya Uswisi ya Stockli yaona Michezo ya Olimpiki ya Beijing kama kichocheo cha biashara yake nchini China

GENEVA – Kampuni ya vifaa vya Michezo ya Uswisi Stockli ambayo ni mtengenezaji mkuu wa vifaa vya michezo ya kuteleza kwenye theluji imesema Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imeongeza nguvu mpya katika biashara yake nchini China na kwamba inatarajia kuona ukuaji wa biashara yake kwa tarakimu mbili katika miaka michache ijayo. "Tunaamini kwamba hata baada ya Olimpiki, mwelekeo wa ukuaji wa michezo ya majira ya baridi nchini China utaendelea," Christian Gut, Afisa Mkuu wa mauzo na masoko katika Kampuni hiyo ya Stockli ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.

“Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inaonesha uthabiti wa michezo katikati ya janga la UVIKO”

DUBAI – Vyombo mbalimbali vya habari vya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu vimeripoti kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inayoendelea mjini Beijing, nchini China imethibitisha kwa Dunia utahimilivu wa michezo katikati ya janga la UVIKO-19. Licha ya changamoto kubwa chini ya hali ya sasa, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing imepata "mwanzo mzuri pamoja na hatua zote zilizowekwa ili kuhakikisha usalama wa wale wanaoshiriki," inasema tahariri ya Gulf News, gazeti la kila siku la Kiingereza huko Dubai.

Eneo la Kitanzi la kudhibiti UVIKO-19 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni thabiti: The Independent

Wanamichezo wakishiriki katika mazoezi kabla ya raundi ya 8 ya mchezo wa Curling kwa Wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kati ya Japani na Korea Kusini katika Kituo cha Taifa cha Kuogelea huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 14, 2022. (Xinhua/Huang Xiaobang) LONDON, Februari 14 (Xinhua) – Gazeti la Uingereza la The Independent limesema kwamba, kuleta zaidi ya watu 15,000 kutoka pembe zote za Dunia hadi Beijing kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kunaleta hatari kubwa ya kuenea UVIKO-19 nchini China.

Iliyopita1 2 3 4 5 6 Inayofuata