人民网首页

Habari

Li Liancheng (kushoto) akizungumza na mkulima mkubwa wa nafaka kwenye mashamba yaliyopangiliwa kwa kigezo cha juu katika Mji wa wilaya Qingzu ya Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan nchini China, Februari 21. (Picha na mwandishi wa Shirika la Habari la Xinhua, Zhang Haoran)

Mjumbe wa Bunge la Umma la China: Siku za furaha bado zinakuja

Kwenye mjadala wa wajumbe wa Mkoa wa Henan wa Bunge la Umma la 13 la China, Li Liancheng ambaye ni mjumbe wa Bunge la 13 la Umma la China akiwakilisha kijiji chake cha Xixinzhuang aliripoti ndoto nane za wakulima kwa Katibu Mkuu wa Chama Xi Jinping. "Wakulima wa China wana ndoto nane.

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Pili wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China hapa Beijing, Mji Mkuu wa China. Mkutano huo wa wajumbe wote umefanyika kuanzia Februari 26 hadi 28, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

Mkutano wa Pili wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC watoa taarifa

BEIJING - Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imetoa taarifa baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Pili wa wajumbe wote siku ya Jumanne. Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu na kuongozwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.

Kamati Kuu ya CPC yafanya mkutano wa mashauriano juu ya mpango wa mageuzi ya vyombo vya Chama na serikali

BEIJING - Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wa mashauriano Jumanne ili kusikiliza maoni na kujulisha vyama vya kisiasa visivyo vya CPC, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) na watu wasio wa chama chochote katika mpango wa mageuzi ya vyombo vya Chama na serikali. Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

Wang Yinxiang (mbele) atambulisha vyakula maalum  vilivyotengenezwa kijijini kwenye chumba cha matangazo ya moja kwa moja mtandaoni Februari 20, katika Kijiji cha Wulidun, Wilaya ya Cao, Mkoa wa Shandong, China. (Picha na mwandishi wa Shirika la Habari la Xinhua, Xu Suhui)

Mjumbe wa Bunge la Umma la China awa “injini muhimu” na kuingiza nguvu mpya katika kustawisha vijiji

Asubuhi ya Machi 8, 2018, Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping alishiriki kwenye mjadala wa ujumbe wa Mkoa wa Shandong kwenye Bunge la Umma la China, ambapo Wang Yinxiang, Mjumbe wa bunge hilo la umma kutoka Kijiji cha Wulidun kilichoko Mkoa Shandong wa China alitoa hotuba papo hapo. Kutoka kijiji maskini hadi kijiji tajiri huko Yexing Jingmei, ni jinsi gani Kijiji cha Wulidun kilipata maendeleo mazuri? Kuchangia akiba, kuongoza wanakijiji kuhamisha umiliki wa ardhi, kuendeleza shughuli za ufugaji, upandaji wa mboga na maua.

Iliyopita7 8 9 10 11 Inayofuata