Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Bunge la Umma la China akikutana na waandishi wa habari walioripoti habari za mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14, na kutoa shukrani zake kwa juhudi zao, katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2025. (Xinhua/Liu Bin) BEIJING - Zhao Leji, Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China jana Jumatano alikutana na waandishi wa habari walioripoti na kutangaza habari za mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14, akitoa shukrani zake kwa juhudi zao.
Mawaziri na viongozi wa Serikali ya China wamehudhuria mahojiano na waandishi wa habari na kujibu maswali mbalimbali kuhusu masuala ya wizara na mamlaka wanazoziongoza jana Jumanne, Machi 12, baada ya kikao cha kufunga mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China.
Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wakihudhuria kwenye mkutano wa tatu wa kufungwa wa Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2025. (Xinhua/Li Xueren) BEIJING – Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, ambalo ni chombo kikuu cha utungaji wa sheria cha China umemalizika jana Jumanne, ambapo Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kwenye mkutano huo wa kufungwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, Li Hongzhong, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano akiongoza kikao cha tatu cha tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei) BEIJING – Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, ambalo ni chombo cha utungaji wa sheria cha kitaifa cha China, imefanya kikao chake cha tatu jana Jumatatu, ambapo akiwa amekaimishwa kazi na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano Li Hongzhong ameongoza kikao hicho.