人民网首页

Habari

Picha hii iliyopigwa Julai 10, 2026 ikionyesha treni ya mizigo kwenye Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi ikiingia katika Stesheni ya Reli ya Port Reitz, Mombasa, Kenya. (Xinhua/Xie Jianfei)

Reli ya SGR ya Kenya yashuhudia ongezeko la mizigo baada ya kuanza kwa sera ya ushuru-sifuri ya China

Tokea Mei 1, China ilianza kutekeleza sera ya ushuru-sifuri kwa bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika ambazo inadumisha uhusiano wa kidiplomasia nazo. Kwa mujibu wa Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Africa Star, Reli ya SGR ya Kenya iliendesha treni za mizigo jumla ya 3,931 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, ikisafirisha tani milioni 4.

Maoni: Kutazama Ufunguaji Mlango na Ushirikiano Kupitia Rekodi Mpya ya Thamani ya Biashara ya China-Afrika Iliyozidi Yuan Trilioni 1

Usiku unapoingia katika mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, China, malori yaliyosheheni matunda freshi yanapita kwa kasi barabarani, yakipeleka matunda matamu kutoka Afrika Kusini kwenye supamaketi na masoko sehemu mbali mbali nchini China. “Kwa ushuru wa forodha kushuka kutoka asilimia 10 hadi sifuri, gharama za uagizaji kwa shehena hii ya tufaha imepungua kwa karibu Yuan 20,000," amesema Luo Shengcong, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Usafirishaji wa Mizigo ya Jianchengye ya Shenzhen.

Jiang Feng, mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika (AU), akitoa hotuba kwenye mkutano wa kutangaza Maonyesho ya 140 ya Canton katika makao makuu ya AU, Addis Ababa, Ethiopia, Julai 7, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Maonyesho ya Canton yatangazwa katika AU ili kuunganisha biashara za Afrika na wanunuzi duniani

ADDIS ABABA - Maafisa kutoka China na Umoja wa Afrika (AU) wamesisitiza umuhimu wa Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Canton, katika kuunganisha biashara za Afrika na wanunuzi, wawekezaji, washirika wa teknolojia, na fursa mpya za kibiashara duniani. Kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano uliofanyika Jumanne wiki hii katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ili kutangaza Maonyesho ya 140 ya Canton.

“China Imeweza Kufanikiwa, na Nchi Zingine Zinazoendelea Zinaweza Kufanikiwa Vilevile”

Kutimiza mambo ya kisasa imekuwa ni jitihada isiyokoma ya watu wa China tangu zama za karibuni, na pia ni matarajio ya pamoja ya watu wa mataifa yote duniani. "China imeweza kufanikiwa, na nchi zingine zinazoendelea zinaweza kufanikiwa vilevile.

Iliyopita4 5 6 7 8 9 Inayofuata