人民网首页

Picha

Matumizi ya RMB yapanuka barani Afrika kutokana na kukua kwa muunganisho wa kifedha na biashara

Wageni wakisherehekea uzinduzi wa huduma ya malipo ya moja kwa moja kwa RMB ya Benki ya Stanbic Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 12, 2026. (Xinhua/Nurdin Pallangyo) NAIROBI - Sarafu ya China, renminbi (RMB), inabeba jukumu kubwa zaidi barani Afrika wakati huu ambapo biashara na Afrika ikistawi.

Zanzibar yawatunuku timu ya madaktari na wataalamu wa kichocho wa China kwa mchango wa huduma ya afya

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikimwonesha Kaimu Waziri wa Afya wa Zanzibar Saada Mkuya Salum (wa pili, kulia) akikabidhi cheti cha heshima kwa kundi la tatu la wataalamu chini ya awamu ya pili ya mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho unaosaidiwa na China, visiwani Zanzibar, Tanzania, Agosti 31, 2026. (Timu ya Wataalamu wa Mradi wa Kuzuia na Kudhibiti Kichocho unaosaidiwa na China/kupitia Xinhua) DAR ES SALAAM - Wizara ya Afya ya Tanzania Zanzibar imewapongeza Kundi la 35 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar na kundi la tatu la wataalamu chini ya awamu ya pili ya mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho unaosaidiwa na China kwa mchango wao kwa sekta ya afya ya visiwa hivyo.

Botswana na kampuni ya madini inayowekezwa na China zashirikiana kuanzisha kituo cha mafunzo ya ufundi

Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, huko Gaborone, Botswana, Agosti 24, 2026. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua) GABORONE - Wizara ya Elimu ya Juu ya Botswana na kampuni ya uchimbaji wa Shaba ya Khoemacau inayowekezwa na China jana Jumatatu wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuanzisha Kituo cha Ubora cha Uchimbaji wa Madini kwenye Chuo cha Ufundi cha Maun katika sehemu ya Kaskazini Magharibi ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ili kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa wafanyakazi wa kiufundi wa sekta ya madini ya nchi hiyo.

Wageni wakikubaliana na Taarifa ya Pamoja ya Jukwaa la 7  la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika lililofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Agosti 20, 2026. (Xinhua/Jin Liwang)

Jukwaa la 7 la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China-Afrika lafanyika Beijing

Jukwaa la 7 la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika lenye kaulimbiu ya "Kunufaika Pamoja na Fursa za Maendeleo, Kujenga Siku za Baadaye za Utangazaji wa TV na Radio" limekuwa likifanyika Beijing, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Julai 19 hadi 21.

1 2 3 4 5 6 下一页