人民网首页

Picha

Waziri wa utalii wa Ushelisheli asema uhusiano kati ya Ushelisheli na China utaimarika zaidi katika kipindi cha miaka 50 ijayo

Waziri wa Utalii na Utamaduni wa Ushelisheli Amanda Bernstein akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Victoria,Ushelisheli, Juni 25, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei) VICTORIA - Waziri wa Utalii na Utamaduni wa Ushelisheli Amanda Bernstein amesema uhusiano kati ya Ushelisheli na China sasa unaingia katika zama mpya ya ushirikiano na maendeleo, hasa katika mawasiliano ya kitamaduni.

Mkoa wa Hunan Katikati mwa China waongeza biashara kati ya China na Afrika kwa uvumbuzi wa sera

Watu wakitembelea banda la Afrika Kusini kwenye Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho na Mikutano cha Changsha mjini Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 12, 2025. (Xinhua/Wang Jingqiang) CHANGSHA – Kwenye soko lenye pilika nyingi mjini Changsha, mji mkuu wa Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, wanunuzi wanachagua bidhaa maalum za Afrika.

Balozi wa Burundi nchini China Télesphore Irambona akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari Juni 12, 2026. (Picha/Song Ge)

Wiki ya Utamaduni wa Burundi kufanyika Beijing

Balozi wa Burundi nchini China, ambaye pia ni mwakilishi wa nchi inayoshikilia uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, Télesphore Irambona, ametangaza kwamba Ubalozi wa Burundi mjini Beijing utafanya Wiki ya Utamaduni wa Burundi ambayo ni ya kwanza kabisa kufanyika, ikihusisha shughuli mbalimbali. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Burundi Juni 12, Balozi Irambona alieleza kuwa mfululizo wa shughuli za Wiki hiyo ya Utamaduni wa Burundi zenye kaulimbiu isemayo "Ngoma Takatifu ya Burundi (Ingoma) Inapoimarisha Uhusiano wa Kiutamaduni kati ya China na Afrika" zitafanyika jijini Beijing kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 1 Julai, zikihusisha kwa sehemu kubwa maonyesho ya kiutamaduni, kongamano la uwekezaji, na maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa Burundi.

Timu ya madaktari ya China yaadhimisha Siku ya Watoto kwa huduma ya matibabu bila malipo nchini Tanzania

Wajumbe wa kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania Bara wakimwelekeza mwanafunzi mbinu za ufufuaji wa moyo na mapafu (CPR) shuleni jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman) DAR ES SALAAM - Kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania Bara limefanya shughuli ya huduma ya matibabu bila malipo jana Jumatatu katika shule jijini Dar es Salaam, likitoa mashauriano na elimu ya afya ya umma bila malipo kwa walimu na wanafunzi.

上一页1 2 3 4 5 6 下一页