Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, huko Gaborone, Botswana, Agosti 24, 2026. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua) GABORONE - Wizara ya Elimu ya Juu ya Botswana na kampuni ya uchimbaji wa Shaba ya Khoemacau inayowekezwa na China jana Jumatatu wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuanzisha Kituo cha Ubora cha Uchimbaji wa Madini kwenye Chuo cha Ufundi cha Maun katika sehemu ya Kaskazini Magharibi ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ili kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa wafanyakazi wa kiufundi wa sekta ya madini ya nchi hiyo.
Jukwaa la 7 la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika lenye kaulimbiu ya "Kunufaika Pamoja na Fursa za Maendeleo, Kujenga Siku za Baadaye za Utangazaji wa TV na Radio" limekuwa likifanyika Beijing, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Julai 19 hadi 21.
Chen Hai, balozi wa China nchini Ethiopia, akizungumza kwenye Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning) ADDIS ABABA - China imezindua Mkutano nchini Ethiopia unaoitwa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" Jumatano wiki hii mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha na kupanua mauzo ya nje ya bidhaa za Ethiopia kwenye soko la China.
Picha hii iliyopigwa Mei 28, 2026 ikionyesha Yuan Gang, mtaalamu wa mionzi katika kundi la 35 la timu ya matibabu ya China visiwani Zanzibar, akijadili picha za MRI na madaktari wenyeji kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, Tanzania. (kundi la 35 la timu ya matibabu ya China visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua) DAR ES SALAAM – Ndani ya chumba cha mionzi katika Hospitali ya Mkoa ya Lumumba visiwani Zanzibar, Tanzania mabadiliko ya kimyakimya ya teknolojia yanabadilisha namna madaktari wanavyobaini magonjwa, kufanya maamuzi, na kuokoa maisha.