Wageni wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya mafunzo baada ya hafla ya uzinduzi, Yaounde, Cameroon, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Kepseu) YAOUNDE – Kampuni ya Uhandisi ya First Highway ya China (CFHEC) imezindua mpango wa mafunzo uliopewa jina la Mpango wa Vipaji wa Seagull jana Jumatatu ili kujenga utaalamu wa wenyeji nchini Cameroon.
Kampuni mbalimbali za China zinashiriki kwenye Maonyesho ya Umeme na Nishati ya Afrika na Maonyesho ya Nishati ya Jua ya Afrika yanayofanyika kuanzia Tarehe 29 hadi 31 Julai jijini Nairobi, Kenya. Kampuni hizo zinaonesha teknolojia mpya na uvumbuzi katika umeme unaozalishwa kwa nishati ya jua, uhifadhi wa nishati na zana na vifaa vya umeme ili kusaidia kuhimiza miundombinu ya nishati barani Afrika ipandishwe ngazi mpya.
ADDIS ABABA - China na Afrika zimezindua mipango ya ushirikiano wa kimatibabu mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia jana Jumatatu, inayolenga kuzifanya huduma za afya ya umma barani humo kuwa za kisasa, ikiwa ni sehemu ya kuzidisha mifumo ya ushirikiano wa kivitendo wa afya ya umma kati ya China na Afrika. Hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Hospitali ya Xiangya ya Chuo Kikuu cha Kusini Kati cha China, Hospitali Kuu ya Silk Road ya Addis Ababa, na Muungano wa Hospitali wa China na Afrika, imeshuhudia uzinduzi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa Tiba ya Upasuaji Kidogo, pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo ya Upasuaji kwa Roboti kati ya China na Afrika na Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Endoskopia kati ya China na Afrika.
NAIROBI - Kiasi cha jumla cha mizigo kilichosafirishwa kwenye ya Reli ya Standard Gauge (SGR) ya Mombasa-Nairobi ya Kenya, mradi kinara chini ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), kimezidi tani milioni 50 kufikia Julai 26, Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Africa Star (Afristar) imesema Jumatatu. Kampuni hiyo imesema tangu kuanza kwa uendeshaji wake Mei 31, 2017, reli hiyo ya SGR ya Mombasa-Nairobi imedumisha rekodi ya uendeshaji salama kwa siku zaidi ya 3,300 mfululizo.