人民网首页

Habari

Bunge la Umma la China lapitia muswada wa sheria wa mpango wa maendeleo ya nchi

BEIJING - Bunge la Umma la China jana Alhamisi lilianza kujadili muswada wa sheria ambao unaweka kanuni za kutungwa na kutekelezwa kwa mpango wa maendeleo ya nchi wa miaka mitano. Muswada huo wa sheria wa mpango wa maendeleo ya nchi uliwasilishwa kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China kwa kujadiliwa na kupitishwa.

Viongozi wa China wahudhuria vikao vya majadiliano kwenye mkutano wa mwaka wa bunge

Li Qiang, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, akijumuika na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Yunnan kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Viongozi waandamizi wa China jana Alhamisi walihudhuria vikao vya majadiliano kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), bunge la kitaifa la China.

Rais Xi ahimiza mikoa yenye uchumi mkubwa kuongeza maarifa ya kutatua matatizo mapya

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ameihimiza mikoa ya China yenye uchumi mkubwa zaidi kufanya juhudi maradufu ili kuongeza maarifa katika kuchambua hali mpya na kutatua matatizo mapya.

Bunge la Umma la China lafungua mkutano wa mwaka

Kikao cha kufungua mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Wang Ye) BEIJING - Bunge la 14 la Umma la China, chombo cha juu cha utungaji sheria cha China, limefungua mkutano wake wa nne leo Alhamisi asubuhi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

1 2 3 4 Inayofuata