人民网首页

Picha

Bunge la 14 la Umma la China lakamilisha mkutano wa mwaka

Bunge la 14 la Umma la China (NPC) likifanya kikao cha kufungwa kwa mkutano wake wa nne katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Bunge la 14 la Umma la China (NPC), chombo cha utungaji sheria cha kitaifa cha China, limekamilisha mkutano wake wa nne jana Alhamisi katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing la China.

Kampuni za umiliki wa mtu mmoja zinazowezeshwa na wakala wa AI zawa mada moto katika "mikutano mikuu miwili" ya China

Fundi (kulia) akizungumza na mtumiaji baada ya kuweka wakala wa AI wa chanzo wazi OpenClaw kwenye kompyuta mjini Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Ji Chunpeng) BEIJING -- "Kufuga kambakoche" (Raising lobster) na kampuni za umiliki wa mtu mmoja (OPCs), ambazo zimezua mijadala mikali katika jamii ya AI ya China na miongoni mwa umma, pia ni mada moto katika "mikutano mikuu miwili" inayoendelea ya nchi hiyo mwaka huu.

Tume ya Utendaji wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China yafanya kikao cha tatu

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), akiongoza kikao cha tatu cha tume hiyo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2026. (Xinhua/Liu Bin) BEIJING – Tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), imefanya kikao chake cha tatu jana Jumatano.

Wajumbe wa mkutano wa Bunge la Umma la China wawasilisha mapendekezo 226 kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo la umma

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sekretarieti ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 10, 2026. (Xinhua/Wang Xi) BEIJING – Wajumbe wa Mkutano wa Bunge la Umma la China wamewasilisha mapendekezo 226 kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China hadi kufikia Jumapili adhuhuri, ambayo ilikuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo kwenye mkutano huo wa nne wa Bunge hilo la Umma unaoendelea mjini Beijing.

1 2 3 4 5 Inayofuata