Maelezo ya Picha: Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea kwanza Afrika kila mwaka mpya kwa miaka 33, Hadithi ya urafiki wa China na Afrika yaendelea (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2023

2. “Mipango Kumi ya Ushirikiano ”, “Hatua Nane” na “Miradi Tisa”

Kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Mwaka 2015, China ilitangaza utayari wake wa kuweka mkazo katika kutekeleza “Mipango Kumi ya Ushirikiano ” pamoja na upande wa Afrika katika miaka 3 inayofuata.

Kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC Mwaka 2018, China ilitangaza kuwa itatekeleza “Hatua Nane” za kusaidia Afrika.

Kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC Mwaka 2021, China ilitangaza kuwa pande hizo mbili zitatekeleza kwa pamoja “Miradi Tisa” ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miaka mitatu ya kwanza ya “Dira ya Ushirikiano kati ya China na Afrika ya 2035”.

 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha