Maelezo ya Picha: Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea kwanza Afrika kila mwaka mpya kwa miaka 33, Hadithi ya urafiki wa China na Afrika yaendelea (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2023

3. Ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” wa China na Afrika wawa mfano wa kuigwa kwa Ushirikiano wa Kusini-Kusini

Mafungamano kati ya China na Afrika yakihimizwa na ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” yameendelezwa kwa kasi.

Tangu FOCAC ilipoanzishwa, makampuni ya China yametumia mitaji ya aina mbalimbali kuzisaidia nchi za Afrika kujenga na kuboresha miundombinu, yamejenga na kukarabati reli zenye urefu wa zaidi ya kilomita 10,000, barabara za urefu wa karibu kilomita 100,000, madaraja karibu 1,000, bandari karibu 100, mtandao wa usambazaji umeme wenye urefu wa kilomita 66,000, mitambo ya umeme yenye uwezo wa kuzalisha kilowati milioni 120, na mtandao wa intaneti unaotoa huduma karibu milioni 700. 

 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha