Maelezo ya Picha: Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea kwanza Afrika kila mwaka mpya kwa miaka 33, Hadithi ya urafiki wa China na Afrika yaendelea (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2023

4. Teknolojia za China zahimiza maendeleo ya kijani ya Afrika

China inaunga mkono kithabiti maendeleo endelevu ya Afrika, na imesaidia kutekeleza mamia ya miradi ya nishati safi na maendeleo kijani chini ya mfumo wa FOCAC.

Reli ya Nairobi-Mombasa nchini Kenya kwa jumla imewekwa njia maalumu 14 kwa ajili ya wanyama pori, na madaraja 79, ili wanyama wakubwa kama tembo na twiga waweze kupita bila matatizo .

Mtambo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua wa Garissa, ambao ni mkubwa zaidi katika Afrika Mashariki, umejengwa na kampuni ya China, na wastani wa uzalishaji wake wa umeme kila mwaka unaweza kukidhi mahitaji ya watu 380,000 kutoka kaya 70,000, na kusadia kupunguza utoaji wa kaboni kiasi cha tani 64,000 kila mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha