Maelezo ya Picha: Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea kwanza Afrika kila mwaka mpya kwa miaka 33, Hadithi ya urafiki wa China na Afrika yaendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang kufuatia mwaliko ametembelea Ethiopia, Gabon, Angola, Benin, Misri, Makao Makuu ya Umoja wa Afrika na Makao Makuu ya Umoja wa Nchi za Kiarabu kuanzia Tarehre 9 hadi 16 Januria.

Huu ni mwaka wa 33 mfululizo ambapo Afrika imekuwa sehemu ya ziara ya kwanza ya kila mwanzo wa mwaka mpya ya waziri wa mambo ya nje wa China nje ya nchi.

Kwanini urafiki kati ya Afrika na China ni wa kina namna hii? Wakati ziara ya mwaka mpya ya waziri wa mambo ya nje wa China imekamilika, hebu tukumbuke pamoja historia nzuri ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, na tutarajie ushirikiano kati ya China na Afrika katika zama mpya ulio katika mwelekeo wa kiwango cha juu zaidi, mwenye kunufaisha zaidi maisha ya watu, na wa endelevu zaidi. 

1. Moyo wa Urafiki na Ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa thabiti zaidi kadri muda unavyopita

Tarehe 30, Mei, 1956 China na Misri zilianzisha uhusiano wa kibalozi, ambao ulifungua milango ya diplomasia ya Jamhuri ya Watu wa China na nchi za Afrika

Tarehe 25, Oktoba, 1971, Mkutano wa Baraza Kuu la 26 la Umoja wa Mataifa (UM) ulipitisha Azimio Na. 2758, ambalo lilirejesha kiti halali cha Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa. Nchi 11 kati ya 23 zilizotoa pendekezo hilo ni nchi za Afrika, na kura za ndiyo 26 kati ya kura 76 zilitoka nchi za Afrika.

Kwa muda mrefu, China na Afrika zimejenga pamoja misingi ya urafiki na ushirikiano ya kuwa na “urafiki wa dhati, kutendeana kwa usawa, kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja kuteteaa haki, kulinda haki, kuendana na mabadiliko ya wakati, na kufungua milango na kuwa na jumuishi.”

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha