Maelezo ya Picha: Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea kwanza Afrika kila mwaka mpya kwa miaka 33, Hadithi ya urafiki wa China na Afrika yaendelea (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2023

5. Chanjo kutoka China zasaidia Afrika kuziba “pengo la kinga”

Baada ya kutokea kwa maambukizi ya UVIKO-19, China na nchi za Afrika zilikabiliana kwa pamoja na janga zikisaidiana na kuungana mkono. Mnamo Februari, 2020, Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika lilitoa taarifa likiunga mkono juhudi za China za kupambana na maambukizi ya virusi vya korona.

Baada ya maambukizi ya UVIKO kutokea Barani Afrika, chini ya ushirikiano wa pamoja, uzalishaji wa chanjo wa China barani Afrika umefikia dozi milioni 400 hivi kila mwaka.

Katika mkutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC Mwaka 2021, China ilitangaza kutoa tena dozi bilioni 1 za chanjo, miongoni mwake kuna dozi milioni 600 za bure, na dozi milioni 400 zitakazotolewa kupitia uzalishaji wa pamoja wa kampuni za China na nchi husika za Afrika. China pia itasaidia nchi za Afrika kutekeleza miradi kumi ya huduma za matibabu na usafi wa kiumma, na kupeleka madaktari na wataalamu wa afya ya umma 1500 kwa bara hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha