Ndege mtilili mwenye koo nyeupe aonekana katika bustani ya Mji wa Xiamen, Kusini Mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2024
Ndege mtilili mwenye koo nyeupe aonekana katika bustani ya Mji wa Xiamen, Kusini Mashariki mwa China
Ndege mtilili mwenye koo nyeupe na picha yake iliyoakisiwa majini ikionesha hali ya kupendeza sana. (People's Daily Online/Chen Bo)

Katika bustani moja iliyo karibu na Ziwa Yundang la Mji wa Xiamen, mkoani Fujian, Kusini Mashariki mwa China, watu wamegundua ndege mmoja wa bluu anayependeza. Ndege huyo anayejulikana kwa jina mtilili mwenye koo nyeupe, anayeonekana kuwa na uchangamfu zaidi, pamoja na manyoya yake ya nyuma ya rangi ya bluu yanayometameta kwenye mwanga wa jua, amewavutia sana watu kwenye bustani hiyo.

Iwe akiwa amepumzika juu ya matawi ya miti, akitazama mazingira yake, au akiwa anaruka kwa madaha juu ya maji, mwonekano wake umewashangaza na kuwavutia sana watalii. Ndege mtilili mwenye koo nyeupe ni spishi iliyo chini ya ulinzi wa serikali wa ngazi ya pili nchini China.

Chen Hao, naibu mkuu wa Shirikisho la Kufuatilia Ndege la Xiamen amefahamisha kuwa, ndege huyo anakula zaidi samaki, kaa, moluska na wadudu wa majini. Ni ndege mkaazi wa Mji wa Xiamen na anaweza kupatikana katika bustani mbalimbali na ardhi oevu.

Mshabiki wa kutazama ndege Bw. An Weiliang amesema, "Ziwa Yundang ni maskani ya ndege wa aina mbalimbali , ikiwa ni pamoja na yangeyange, korongo, na korongo wa usiku. Hata hivyo, kuweza kumwona ndege mtilili mwenye koo nyeupe ni nadra. Ndege hawa wanapendelea kuwa peke yao na mara nyingi wakiwa wamejificha kati ya matawi ya miti karibu na ukingo wa maji. Mara kwa mara, wanaruka na kupiga chenga kwa haraka kwenye maji, na hivyo kufanya iwe vigumu kuwapiga picha bila vifaa vya kitaaluma" .

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha