Kampuni ya magari ya BYD ya China yapata mafanikio katika soko la magari la Sri Lanka (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 28, 2025
Kampuni ya magari ya BYD ya China yapata mafanikio katika soko la magari la Sri Lanka
Wawakilishi wa BYD na Kampuni ya usambazaji wa Magari ya John Keells CG wakionyesha MoUs ili kuwezesha chapa ya kifahari ya BYD ya DENZA kuingia katika soko la ndani mjini Colombo, Sri Lanka, (Picha na Ajith Perera/Xinhua)

COLOMBO - BYD, kampuni ya magari ya nishati mpya (NEV) ya China, inapanua uwepo wake nchini Sri Lanka kwa mipango ya kutambulisha DENZA, chapa yake ya kifahari ya hali ya juu, kupitia kampuni msambazaji magari ya nchini humo ya John Keells CG.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Colombo jana Jumanne, wawakilishi wa BYD na John Keells wametia saini Waraka wa Makubaliano (MoU) kuwezesha kuingia kwa DENZA katika soko la ndani, ikionyesha nia yao ya kupanua soko la magari yanayotumia umeme ya hali ya juu nchini Sri Lanka.

DENZA, iliyoanzishwa mwaka 2010, inajikita katika uundaji wa magari yanayotumia nishati mpya ya kifahari na modeli zake za sasa ni pamoja na D9, N7, Z9, na Z9GT, ikiahidi watumiaji wa Sri Lanka watapata uzoefu mzuri zaidi wa usafiri kwa pande zote.

Akizungumza katika hafla hiyo, Krishan Balendra, mwenyekiti wa Kundi la Kampuni za John Keells, amesema mafanikio ya haraka ya BYD katika sekta ya NEV ya Sri Lanka "yanaonyesha nguvu ya ushirikiano wetu na matumaini wetu pamoja kwa mustakabali wa baadaye wa vyombo vya usafiri."

Tangu Sri Lanka ipunguze vizuizi vya kuagiza bidhaa mapema mwaka 2025, BYD imevutia watumiaji kwa haraka kwa aina mbalimbali za magari yanayotumia nishati mseto ya umeme na mafuta. Kuongezeka kwa mahitaji ya magari ya BYD kunaonyesha mabadiliko ya watumiaji kuelekea vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati mpya nchini Sri Lanka.

Ili kuimarisha zaidi uwepo wake wa soko, BYD na John Keells CG zinapanua haraka maeneo yao ya kuuza magari na mitandao ya huduma baada ya mauzo.

Maeneo hayo yanatazamiwa kufunguliwa hivi karibuni katika miji ya Ampara na Ratnapura katika mikoa ya Mashariki na Sabaragamuwa ya Sri Lanka, mtawalia.

Liu Xueliang, meneja mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha BYD Tawi la Asia-Pasifiki, amesema Sri Lanka ni soko muhimu kwa BYD katika Asia ya Kusini.

"Wakati ukubwa wa biashara nchini Sri Lanka hauko katika kiwango sawa na masoko mengine ambayo tumeingia katika kanda hiyo, ukubwa wa Sri Lanka unamaanisha kuwa bado inaweza kutumika kama utafiti wa mfano wa dunia kwa matokeo chanya ya vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme katika kiwango cha kitaifa." amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha