

Lugha Nyingine
China inayosonga mbele | Miti iliyojeruhiwa yatoa manukato ya ajabu: Kuchunguza siri ya ufundi uliorithiwa wa Guangdong
Katika Hifadhi ya Miti ya Ubani ya Guanxiang kwenye Daliangshan mjini Dongguan, Mkoa wa Guangdong, China, miti ya ubani inasimama kimya. Guanxiang, ni ubani adimu unaozalishwa kwa utomvu unaotoka kwenye miti ya ubani iliyojeruhiwa. Inajulikana kama “hazina ya Lingnan” kwa “manukato yake safi inayohisika kwa mbali na uwezo mkubwa wa kimatibabu.”
Meneja wa hifadhi hiyo ameeleza kuwa, mji wa Dongguan una hali ya hewa ya wastani na yenye unyevu, na mazingira yake kipekee ya vilima vidogovidogo hutoa ardhi nzuri kwa miti hiyo kuzalisha ubani.
Kwa sasa, Guanxiang umeingia maisha ya kisasa. “Mji mdogo wa Guangxiang” katika Dalingshan unashirikana na mashamba, majumba ya makumbusho na vituo vya biashara. Uzalishaji wa mwaka wa ubani zaidi ya tani 3 hutengenezwa kuwa mafuta na bidhaa za ngozi, zikifikia wanunuzi; Madarasa ya ujuzi wa ubani, na kushiriki burudani ya kuvuna utomvu wa miti huvutia watalii vijana...
Manukato hayo ambayo yamesafiri kupita maelfu ya miaka kwa sasa yanaendelea kwa sura mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma