China na Misri zasaini makubaliano juu ya uendeshaji wa Eneo la CBD katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2025
China na Misri zasaini makubaliano juu ya uendeshaji wa Eneo la CBD katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala
Picha hii iliyopigwa Oktoba 21, 2024 ikionyesha mwonekano wa usiku wa Eneo la Katikati la Kibiashara (CBD) la mji mkuu mpya wa utawala wa Misri, mashariki mwa Cairo, Misri. (Xinhua/Wang Dongzhen)

CAIRO - Mamlaka ya Jumuiya za Mijini mipya ya Misri na kampuni ya ubia kati ya China na Misri wametia saini makubaliano ya uendeshaji na utengenezaji wa pande zote kwa ajili ya Eneo la Katikati la Kibiashara (CBD) katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala wa Misri.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Kampuni ya Horizon Operations Management (Egypt) itawajibika kwa uendeshaji wa mradi huo wa CBD, mwanzoni ikitilia maanani katika usimamizi wa nyumba na manispaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya baraza la mawaziri la Misri, Waziri wa Makazi wa Misri Sherif El-Sherbiny amesema wakati wa mazungumzo ya kabla ya kutia saini kwamba makubaliano hayo yanahusu utengenezaji na usimamizi wa miundombinu muhimu na utoaji wa huduma za mijini kwa wakaazi, watalii na makampuni katika CBD.

El-Sherbiny amesisitiza kuwa hatua hiyo inawakilisha mpito muhimu katika namna ya Misri ya kusimamia mradi wa umma -- kutoka njia ya jadi hadi usimamizi wenye msingi wa ufanisi unaozingatia ubora na uendelevu.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika Jumapili ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijijini wa China Dong Jianguo, na wawakilishi wa Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la Serikali ya China, ambalo liliongoza ujenzi wa CBD hiyo.

Likiwa linapatikana katikati ya jangwa umbali wa kilomita karibu 50 mashariki mwa mji mkuu Cairo, eneo hilo la CBD ni moja ya miradi muhimu ya ujenzi wa pamoja wa China na Misri wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Mradi huo ni pamoja na majumba 20 ya maghorofa marefu ya kibiashara na makazi vilevile miundombinu mingine ya manispaa, miongoni mwao ni ghorofa kinara la kuvutia lenye urefu wa juu wa mita 385.8, jengo refu zaidi barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha