

Lugha Nyingine
Uganda yasherehekea Sikukuu ya Mashua ya Dragoni ya China katika Ziwa Victoria (4)
![]() |
Afisa wa Utalii wa Uganda James Mboijana akihutubia shughuli ya mashindano ya mbio za mashua ya dragon mjini Kawuku, wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Juni 1, 2025. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua) |
WAKISO – Juni inapoanza na msimu wa mvua nchini Uganda unapokaribia kuisha hatua kwa hatua, anga juu ya Ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi la maji baridi barani Afrika, hubadilika kati ya mwanga angavu wa jua na mvua ya rasharasha. Lakini si mabadiliko hayo ya hali ya hewa wala umbali kutoka mahali pake pa asili vinaweza kufifisha Sikukuu ya mwaka huu ya Mashua ya Dragoni, iliyosherehekewa Jumapili mjini Kawuku, katika wilaya ya kati ya Uganda ya Wakiso.
Mdundo wa ngurumo wa ngoma ulikuwa ukisikika kwenye maji, ukihimiza wapiga makasia kusonga mbele. Wapiga makasia Waganda na Wachina walifanya kazi bega kwa bega, wakiendesha mashua za dragoni zilizopambwa kuelekea mstari wa kumalizia.
Watazamaji kutoka mabara tofauti, Wachina, Waganda, Wazungu na watu wa nchi mbalimbali za Afrika, walikuwa wakishangilia kutoka ufukweni. Watoto walikuwa wakikimbia kando ya ziwa, wakicheza kufuata mdundo wa ngoma za Kiafrika, huku familia zikichagua kuonja vyakula vya Kichina, kunywa chai za jadi, na kupiga picha za selfie mbele ya vichwa vya mashua ya dragoni na bendera.
Shughuli hiyo ya kila mwaka, ambayo husherehekea Sikukuu ya jadi ya China ya Mashua ya Dragoni, imekuwa jukwaa la mawasiliano ya kitamaduni nchini Uganda. Sikukuu hiyo, ambayo pia inajulikana kwa jina la Sikukuu ya Duanwu, kwa kawaida huangukia siku ya tano ya mwezi wa tano katika kalenda ya kilimo ya China. Mwaka huu, iliadhimishwa Mei 31.
Gloria Asiimwe, akihudhuria shughuli hiyo kwa mara ya kwanza, amesema hawezi kukosa kwa sababu ya kupenda utamaduni wa Wachina.
"Imenibidi nije kwa sababu napenda jinsi Wachina wanavyojibeba. Napenda utamaduni wao, mshikamano wao, tabia zao, kila kitu kuhusu wao," amesema Asiimwe, ambaye pia ni mwanafunzi wa lugha ya Kichina.
Moja ya timu katika mashindao ya mwaka huu ya mashua ya dragoni, ambayo kwa kawaida hupamba sikukuu hiyo, ni Hebei Tiantang, ambayo nahodha wake, Emmanuel Mbaziira, ameelezea furaha yake baada ya kushinda mbio hizo.
“Huu ni mwaka wa tano tunashiriki katika mbio hizi za mashua, na tuna furaha kwamba hatimaye tumeshinda,” Mbaziira amesema. "Tumejifunza mambo mengi kutoka kwa Wachina, na wamejifunza kutoka kwetu."ameongeza
Timu nyingine iliyofuatiliwa sana ni timu ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina wa Taizhou nchini Uganda, ambayo imekuwa ikishiriki tangu kuanzishwa kwa mbio hizo nchini Uganda.
"Mashua za dragoni ni ishara ya ustaarabu wa China," amesema. "Kuleta utamaduni huu nchini Uganda, na kuona wapiga kasia wa China na Uganda wakiwa wameshirikiana pamoja katika boti moja, kuna maana kubwa," amesema Ruan, ambaye jumuiya yake ilinunua boti hizo za dragoni kutoka China kwa mashindano ya kwanza ya mbio hizo nchini Uganda mwaka 2017.
Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong, afisa wa utalii wa Uganda James Mboijana, na wageni wengine kwa pamoja walifanya shughuli ya jadi ya "kuweka alama kwenye macho ya dragoni".
"Kama tu vile wapiga makasia katika mashua moja wakishindana kuelekea lengo moja, China na Uganda zinafanya kazi bega kwa bega kuelekea ujenzi wa mambo ya kisasa," balozi huyo amesema alipokuwa akihutubia shughuli hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma