Mashindano ya Baiskeli ya mzunguko wa Ziwa Sayram ya 2025 yakamilika mjini Xinjiang, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2025
Mashindano ya Baiskeli ya mzunguko wa Ziwa Sayram ya 2025 yakamilika mjini Xinjiang, China
Waendesha baiskeli wakiwa katika raundi ya tano ya mashindano ya mbio za baiskeli ya mzunguko wa ziwa Sayram ya 2025 katika Eneo Linalojiendesha la Kabila la Wamongolia la Bortala, Mkoa wa Xinjiang, China, Juni 4, 2025. (kupitia Xinhua)

URUMQI – Mashindano ya 17 ya Mbio za Baiskeli za mzunguko wa Ziwa Sayram ya 2025 yamehitimishwa jana Jumatano katika Eneo Linalojiendesha la Kabila la Wamongolia la Bortala la Mkoa wa Xinjiang, China, huku waendesha baiskeli kutoka Team BATTLE wakinyakua mataji ya jumla na ya timu baada ya raundi tano zenye changamoto za kuendesha baiskeli sehemu mbalimbali za mkoa huo wa Xinjiang.

Mbio hizo za siku tano zilianza Mei 31 katika Wilaya ya Jinghe na zilikuwa na raundi tano ambazo zilipitia Mji wa Alashankou, Mji wa Bole na Wilaya ya Wenquan kabla ya kuhitimishwa kwenye eneo la kivutio la Ziwa Sayram.

Zikichukua jumla ya umbali wa kilomita 435, mbio hizo zimevutia timu zaidi ya 70 na waendesha baiskeli zaidi ya 380 kutoka sehemu mbalimbali za China na nje ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha