

Lugha Nyingine
Profesa ashuhudia ottelia acuminata ikichanua tena katika Ziwa Erhai, China (6)
![]() |
Mboga freshi ya ottelia acuminata iliyohifadhiwa ikionekana katika picha kwenye Chuo cha Kilimo na Biolojia cha Chuo Kikuu cha Jiao Tong cha Shanghai Mei 29, 2025. (Xinhua/Liu Ying) |
SHANGHAI - Kong Hainan ni profesa mwenyekiti na msimamizi wa tasnifu za wanafunzi wa shahada za uzamivu katika Chuo Kikuu cha Jiao Tong cha Shanghai na pia ni mkuu wa mradi mkubwa wa sayansi na teknolojia wa udhibiti na usimamizi wa uchafuzi wa maji kwenye Ziwa Erhai katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China. Alikuwa akiongoza timu yake kufanya kazi katika mkoa huo kwa miaka karibu 20 ili kuboresha maji ya Ziwa Erhai.
Mimea ya ottelia acuminata, inayojulikana kama kiashirio cha ubora wa maji, ambayo iliwahi kuchanua kwenye Ziwa Erhai. Tangu miaka ya 1990, kutokana na sifa ya maji ya ziwa hilo iliyozidi kuwa mbaya, mmea huo ulikuwa vigumu kupatikana kwenye ziwa. Shukrani kwa juhudi za timu ya Profesa Kong na mamlaka za mitaa, sifa ya maji ya Ziwa Erhai imeboreshwa hatua kwa hatua, na mmea huo wa ottelia acuminata sasa umestawi tena.
Mwaka 2020, Profesa Kong alistaafu akiwa na umri wa miaka 70. Alichukua akiba yake binafsi kwa kuanzisha mfuko wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kwa ajili ya ulinzi wa Ziwa Erhai na kuunga mkono utafiti wa kisayansi juu ya uhifadhi wake.
Katika miaka ya hivi karibuni, ukubwa wa eneo la kilimo cha mimea ya ottelia acuminata ya kuzalishwa na binadamu mkoani Yunnan umefikia hekta 200, na mmea huo umekuwa mboga muhimu kwa watu wenyeji.
Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai pia kwa mafanikio kimeendeleza teknolojia hiyo ya uhifadhi na ulinzi wa ottelia acuminata, na kuhakikisha ubora wake unadumu kwa siku 14. Mboga hiyo ya majani sasa imekuwa chakula maarufu kwenye meza za chakula katika miji mbalimbali nje ya Yunnan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma