Binti afuata nyayo za baba yake kustawisha kijiji alikozaliwa katika Mkoa wa Liaoning, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2025
Binti afuata nyayo za baba yake kustawisha kijiji alikozaliwa katika Mkoa wa Liaoning, China
Li Mingming (kulia) akizungumza na mfanyakazi ndani ya banda la ng'ombe kwenye eneo maalumu la viwanda katika Kijiji cha Arxiang cha Wilaya ya Zhangwu ya Mji wa Fuxin wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China, Juni 3, 2025. (Xinhua/Pan Yulong)

Li Mingming, katibu wa Kamati ya Chama ya Kijiji cha Arxiang cha Wilaya ya Zhangwu ya Mji wa Fuxin wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China, ni mzaliwa wa Arxiang. Baba yake Li Dongkui ni mlinzi na mtunzaji mashuhuri wa misitu.

Kwa sababu ya kazi ya baba yake, Li Mingming hakuweza kumuona baba yake mara nyingi alipokuwa mtoto, kwani wakati fulani baba yake aliishi katika eneo la msitu wa mbali lililokuwa halina ufikiaji wa maji, umeme na njia. Hapo zamani, Li Mingming hakuelewa kabisa chaguo hilo la kazi la baba yake.

Siku za nyuma, Kijiji cha Arxiang kilikumbwa na hali mbaya ya kuenea kwa jangwa na kusababisha mapato chini ya wenyeji. Wakati Li Mingming alipokuwa akikua, mazingira ya ikolojia ya kijiji hicho yaliboreka sana, ikimfanya aelewe umuhimu wa kazi hiyo ya baba yake ya kuwa mlinzi wa misitu.

Akihamasishwa na baba yake, Li Mingming alirudi kijijini hapo alikozaliwa kufanya kazi baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu cha misitu.

Sasa Li Mingming ameongoza wanakijiji kuanzisha eneo maalumu la viwanda jumuishi la "upandaji, ufugaji na utengenezaji wa mazao ya kilimo". Mabanda ya kijani ya kilimo cha kisasa katika eneo hilo yanazuia kwa ufanisi kuenea kwa mchanga huku yakiongeza mapato ya wakulima. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha