Maonyesho ya Raslimali za Mawe ya Kimataifa ya Kunming China 2025 yafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2025
Maonyesho ya Raslimali za Mawe ya Kimataifa ya Kunming China 2025 yafunguliwa
Mtoto wa kike akichagulia wazazi wake kito cha jade kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Rasilimali za Mawe ya Kunming China 2025 huko Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Julai 10, 2025. (Xinhua/Chen Xinbo)

Maonyesho ya Raslimali za Mawe ya Kimataifa ya Kunming China 2025 yamefunguliwa huko Kunming, mji mkuu wa Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China jana Alhamisi. Maonyesho hayo ya siku 5 yanachukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takriban 50,000, yakikusanya jumuiya za wafanyabiashara na vikundi vya maonyesho zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha