Wanasayansi wa China watengeneza roboti ya kwanza duniani inayosaidia mchakato wa kilimo cha mbegu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2025
Wanasayansi wa China watengeneza roboti ya kwanza duniani inayosaidia mchakato wa kilimo cha mbegu
Roboti ya GEAIR inaendelea kufanya kazi ya uchavushaji kwenye banda la kupanda nyanya mjini Beijing, China, Novemba 29, 2024. (IGDB ya CAS/Picha kwa Xinhua)

Wanasayansi wa China hivi karibuni wameunda roboti ya kwanza duniani yenye uwezo wa kusaidia uchavushaji, ikionyesha ushirikiano wa kina wa teknolojia ya kibioteknolojia na teknolojia ya AI katika sekta ya kilimo cha mbegu.

GEAIR, ni jina la modeli mpya ya roboti yenye msingi wa AI, ambayo inatarajiwa kuwezesha mabadiliko ya kazi ya kuandaa mbegu kutokana na kilimo kinachotegemea uzoefu hadi kilimo cha kisasa chenye usahihi.

Hali ambayo zamani ilikuwa kwenye filamu za kisayansi za kufikirika, sasa limekuwa ni jambo halisi linalofanyika kwenye mabanda ya kilimo, ambapo roboti ya GEAIR inatambua ua kwa usahihi na kupanua mikono yake ili kukamilisha uchavushaji kwa upole. Roboti hiyo ilitembea kwa kasi kati ya maua na kufanya kwa usahihi mchakato mzima wa kazi ya kuandaa mbegu. 

Mtafiti wa IGBD Bw. Xu Cao anasema,"AI na roboti vinatoa fursa kubwa katika kubadilisha kazi ya kuandaa mbegu kwenye sekta ya kilimo kuwa sahihi, ili kuongeza mavuno ya mazao, kupunguza gharama na kuhimiza mazoea endelevu.”

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha