Ghana yaandaa maonyesho ya sekta ya matibabu ya China na Afrika Magharibi ili kuhimiza ushirikiano wa matibabu kwa kutumia Akili Bandia (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2025
Ghana yaandaa maonyesho ya sekta ya matibabu ya China na Afrika Magharibi ili kuhimiza ushirikiano wa matibabu kwa kutumia Akili Bandia
Mwanamke akijaribu bidhaa ya ukaguzi wa AI katika Maonesho ya Sekta ya matibabu na Afya ya China-Afrika Magharibi mjini Accra, Ghana, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Seth)

ACCRA, Agosti 21 (Xinhua) – Maonesho ya Pili ya Sekta ya Matibabu na Afya ya China na Afrika Magharibi yamefunguliwa mjini Accra, Ghana, ili kuhimiza matumizi ya akili bandia (AI) katika uchunguzi wa kimatibabu na kuimarisha ushirikiano kwenye miradi ya afya kati ya China na nchi za Afrika Magharibi.

Maonyesho hayo ya siku tatu, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Afya ya Afrika Magharibi (HCOWA), kampuni ya China yenye makao yake makuu nchini Ghana, na Idara ya Afya ya Ghana, ambapo maofisa wa serikali, wataalamu wa afya, wadhibiti, na waonyeshaji zaidi ya 100 kutoka China na nchi mbalimbali za Afrika Magharibi wamekusanyika pamoja kwenye maonesho hayo.

Mkuu wa HCOWA Bw. Jiang Sihong amesema kwenye hafla ya ufunguzi kwamba wakati teknolojia ya AI ikileta mapinduzi kwenye sekta ya afya duniani kote, ni lazima Afrika Magharibi isibaki nyuma ya maendeleo na pia inapaswa kutumia Akili bandia kuboresha utoaji wa huduma za afya ili kukidhi mahitaji ya watu wake.

Bw. Jiang amesema HCOWA iko tayari kushirikiana na wizara, hospitali, na sekta binafsi ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, utafiti na upatikanaji wa huduma za afya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha