Ujenzi wa mfereji wa Pinglu waendelea vizuri mjini Qinzhou Mkoani Guangxi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2025
Ujenzi wa mfereji wa Pinglu waendelea vizuri mjini Qinzhou Mkoani Guangxi, China
Picha iliyopigwa kwa droni Agosti 24, 2025 inaonyesha eneo la ujenzi wa daraja kwenye Mfereji wa Pinglu huko Qinzhou, Mkoani Guangxi, China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Ujenzi wa Mfereji wa Pinglu unaendelea katika hali ya pilikapilika zaidi, na wajenzi wameshinda changamoto mbalimbali zinazosababishwa na joto kali, kimbunga na mvua kubwa ili kuhakikisha ujenzi unaendelea kama ilivyopangwa.

Ukiwa ni mradi muhimu wa Njia Mpya ya Kimataifa ya Biashara ya Ardhini na Baharini, Mfereji wa Pinglu una urefu wa takriban kilomita 134.2, ukivuka miji ya Nanning na Qinzhou iliyoko katika mkoa wa Guangxi nchini China na kutiririka hadi kwenye Ghuba ya Beibu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha